Search This Blog

SportsRaw

SportsRaw

Tuesday, 10 October 2017

Crouch atinga Guiness world Record







Mshambuliaji wa klabu ya Stoke ya England Peter Crouch ameingizwa kwenye kitabu cha rekodi za dunia cha Guinness World Records cha mwaka 2018 kwa kufunga mabao mengi zaidi kwa kichwa Ligi ya kuu ya soka ya England .

Crouch amefunga mabao 51 kwa kichwa katika ligi hiyo, mabao matano zaidi ya gwiji wa zamani wa Blackburn na Newcastle Alan Shearer.
Crouch, 36, kwa jumla amefunga mabao 105 Ligi Kuu ya  katika mechi 436 alizochezea jumla ya klabu sita ligi hiyo.
"Iwapo wewe ni mshambuliaji wa kati, unafaa kuwa eneo la hatari, tayari kufunga bao kwa kichwa," amesema Crouch.
"Hivi ndivyo nimekuwa nikicheza na hilo sitawahi kulibadilisha. Washambuliaji wa kati wakaokaa nje ya eneo la hatari hunishangaza sana, siwezi kuelewa huwa wanafikiria nini"
hivi karibuni Crouch alifunga bao la kichwa dhidi ya Southmpton likiwa ni goli la shindi kwenye mechi ya PL.

0 comments:

Post a Comment