Michuano ya kombe la mapinduzi imeendelea kushika kasi leo katika hatua ya makundi na leo kushuhudia mchezo wa kundi A na kuzikutanisha URA ya Uganda dhidi ya mnyama Simba, katika mechezo huo vijana wa msimbazi amefanikiwa kupata ushindi wa 1-0
![]() |
Mshambuliaji wa timu ya SimbaHamisi (kushoto) kiiza akijaribu kumiliki mpira dhidi y mlinzi wa timu ya URA ya Uganda katika mchezo kombe la Mapinduzi uliofanyika katika uwanja wa Amaan Zanzibar |
Goli la simba limefungwa na Ibrahim Ajibu katika kipindi cha kwanza dakika ya 37baada ya kupata pasi safi kutoka kwa kiungo Mwinyi Kazimoto na na kufanikiwa kuongoza kundi hilo wakiwa na pointi 4 baada ya mechi mbili na wanafuatiwa na URA wenye pointi 3 sawa na JKU na Jamhuri wanashika mkia wakiwa na pointi moja.
![]() |
Ibrahimu Ajibu (kushoto) akishangalia baaada ya kuifungia timu yake goli dhidi ya URA |
0 comments:
Post a Comment