Ligi Kuu Bara inatarajiwa kuendelea leo Jumamosi kwa michezo mitatu mnyama Simba anayeongoza katika msimamo wa ligi itaikaribisha Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Mchezo mwingine utakuwa ni kati ya JKT Ruvu na Mwadui ya Shinyanga mchezo utakaofayika Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani ambako utachezeshwa na Mwanamama mwamzi mwenye beji la FIFA, Mwanahamisi Matiku wa Dar es Salaam.
Stand United ya Shinyanya itaikaribisha African Lyon kwenye Uwanja wa CCM Kambarage katika mchezo .
Ligi hiyo itaendelea kesho Jumapili kwa mchezo utakaozikutanisha timu za Azam na Young Africans; zote za Dar es Salaam. Mwamuzi wa mchezo huo atakuwa Israel Nkongo wa Dar es Salaam.
Ruvu Shooting na Mbeya City Jumapili watatoana jasho kwenye Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani.
Mtibwa Sugar ya Morogoro na Tanzania Prisons ya Mbeya nazo zitacheza Jumapili Oktoba 16 kwenye Uwanja wa Manungu mkoani Morogoro. .
Toto African ya mwanza dhidi ya Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
0 comments:
Post a Comment