Mchezaji asie ishiwa na vituko ndani ya uwanja na nje, Super Mario Balotelli amekosa penalti jana usiku wakati timu ya Nice ilopokuwa inacheza dhidi ya Lyon kwenye mchezo wa ligi 1, Nice ambao wapo katika kiwango bora waliibuka na ushindi wa 2-0
![]() |
Mario Balotelli |
Balotelli ambaye amejiunga na Nice msimu akitokea Liverpool amekuwa katika fomu nzuri katika ligi 1 licha ya kukosa mkwaju wa Penalti katika dakika 81'.
Kwa matokeo hayo Nice wanandelea kujikita kileleni kwa kufikisha Pointi 23 baada ya kushuka dimbani mara tisa, Monaco wapo nafasi ya pili kwa pointi 19 baada ya michezo tisa.
Katika mechi hiyo magoli ya Nice yalifungwa na Baysee 5, Seri 76 Ligi hiyo inaendelea leo na kesho katika viwanja mbalimbali.
![]() |
Super Mario Balotelli (wa tatu kutoka kushoto) akishangilia goli na wachezaji wa Nice |
0 comments:
Post a Comment