Winga hatari watimu ya Yanga Simon Msuva juzi amefikisha magoli 50 tangu ajiunge na wanajangwani msimu wa 2013/14 alifunga goli hilo kwenye ushindi wa 3-1 dhidi ya Mtibwa Sugar amesema lengo lake ni kuhakikisha anafikisha magoli 100.
Wakati akigusia kuhusu kufikisha idadi hiyo ya mabao, pia amegusia suala la yeye kuondoka Yanga na kusema kuwa ikitokea ikawa hivyo nia yake ni kwenda nje ya nchi kucheza na siyo kuhamia Simba au Azam FC ambazo ni klabu kubwa pia kwa hapa nchini.
“Nataka nipambane nifunge mabao mengi zaidi, ikiwezekana 100, ili siku nikiondoka Yanga, niwe na heshima, unajua haya ni maisha siwezi kuwa Yanga siku zote, ipo siku nitaondoka, lakini nataka kufunga mabao mengi na nikiondoka niwe na heshima ili siku nikirejea iwe rahisi wao kunikubali alisema Msuva.
Friday, 14 October 2016
Baada ya 50 Msuva ataka 100
Msuva alisema anashangaa mashabiki wa timu yake kuonyesha kukosa uvumilivu pindi wanapoona mambo yamekaa vibaya na kufikia hatua ya kumzomea, amedai ameshaizoea hali hiyo na haimsumbui.
“Najua mimi ni mchezaji mzuri ndiyo maana napata matokeo mengi kutoka kwa mashabiki ninapokuwa uwanjani, kunizomea au kunipigia kelele naona ni moja ya changamoto za kunirekebisha, hii haimtokei kila mchezaji, hata Ulaya kuna baadhi wanafanyiwa hivi na ni wale ambao wanaonekana wanakosea wakati hawastahili kukosea.
0 comments:
Post a Comment