Meneja wa Simba ambaye pia ni straika wa zamani wa timu hiyo, Mussa Mgosi, amesema wana kila ya sababu ya kuuchukua ubingwa wa ligi kuu msimu huu, kwani wamesajili wachezaji wanaoweza kupambana.
Kauli hiyo ya Mgosi imekuja baada ya Simba kucheza mechi nane hadi sasa na kufikisha pointi 20 huku ikiwa haijapoteza hata mchezo mmoja, kwani ina sare mbili na imeshinda mara sita.
Ukiachana na Kichuya na Mwanjale, msimu huu Simba pia imewasajili Muzamiru Yassin, Laudit Mavugo, Jamal Mnyate, Mousa Ndusha, Besala Bokungu, Mohamed Ibrahim, Malika Ndeule, Fredric Blagnon na Hamad Juma ambao wameonekana kuibeba simba msimu huu
Kutokana na hali hii, tuna matumaini makubwa ya kuuchukua ubingwa msimu huu.”
Mgosi alisema, wigo huo mpana wa kikosi umesababisha kutokuwepo kwa mchezaji tegemeo katika timu, hivyo mtu akiumia basi kunakuwepo na mbadala wake mwenye uwezo kama aliyetoka.
0 comments:
Post a Comment