Wakiwa nyumbani leo Etihad stadium Manchester City wameshindwa kutamba mbele ya Everton baada ya kulamishwa sare ya 1-1 lakin vijana Pep Guardiola watajilaumu wenyew kwani walifanikiwa kupata mikwaju ya penalti miwili na kuishia kukosa yote.
Wakiingia na kumbukumbu ya kichapo kutoka kwa Tottenham Hotspurs 2-0 City leo walihitaji kupata matokeo ili waendelee kukaa kileleni mwa Epl.
Mlinzi wa kati wa Everton Phil Jagielka alimwangusha David Silva na Kevin De Bruyne akapewa jukumu la kupiga akakosa
Romeo Lukaku akapiga bao safi kipndi cha pili bao hilo likawaamsha city usingizini na kuanza kuliandama lango la vijana wa Koeman, wakafanikiwa kupata penalti nyingine safari mpigaji akawa Sergio Aguero ambae mkwaju wake ulipanguliwa na kipa Stekelenberg.
aliewakoa Man city ni mshambuliaji wa kimataifa wa Uhispania Nolito aliefanya mchezo kuisha kwa 1-1
kwa matokeo hayo City wapo kileleni na wanafikisha pointi 19 sawa na Arsenal wakiwa wanatofautiana magoli ya kufungwa na kufunga
Saturday, 15 October 2016
Man City wabanwa mbavu na Everton
Saturday, October 15, 2016
No comments
0 comments:
Post a Comment