Wakiwa kwenye kiwango kizuri mabingwa wa Ulaya Real Madrid jana usiku walifanikiwa kupata ushindi dhidi ya Real Betis kwa kuifunga 1-6 ushindi huu umesitisha matokeo ya sare nne mfululizo huku Madrid wakitandaza soka safi.
Wali droo dhidi ya Villarreal, Las Palmas, Borussia Dortmund na Eibar kocha Zinedine Zidane alikuwa kwenye presha kubwa ya kuhakikisha wanapata matokeo, baada ya mechi Zizuo alikiri hajawahi kuona timu yake inaanza mchezo kwa morali ya juu na kusema matatitzo ya kisaikolojia yalikuwa yanawasumbua vijana wake.
Beki aliechukua nafasi ya nahodha Sergio Ramos, ambaye ni majeruhi Raphael Varane alianza kufungua ukurasa wa magoli Karim Benzema akafunga la pili, beki wa kushoto Marcelo akaipatia la tatu,na kuungo mshambualiji Isco akifunga magoli mawili kabla Cristiano Ronaldo kuhitimisha karamu hiyo ya magoli kwa kuzifumania nyavu kwa mara ya sita
Katika mechi nyingine Atletico Madrid walipata ushindi mnono wa magoli 7-1 walipokuwa nyumbani dhidi ya Granada magoli yalifungwa na Ferreira aliepiga hat-trick 34' 45' 61' Gaitan akafunga mawili 63' 81' dakika tatu baadae Correa alifunga nae 85 ' na Tiago akahitimisha la saba 87'.
kwa matokeo ya jana Atletico Madrid na Real Madrid wapo sawa kwa kfikisha pointi 18, wakwa kileleni na wanatofatiana magoli ya kufunga nafasi ya tatu wapo Sevilla na 17 na Barcelona baada ya ushindi wa jana wanashikilia nafasi ya nne na pointi 16 katika La Liga.
0 comments:
Post a Comment