Timu za Simba na Yanga jana zimefanikiwa kushinda kwenye michezo yao ya Ligi kuu ya Vodacom mnyama alicheza dhidi ya Mbeya city kwenye dimba la Sokeine Mbeya wakati Yanga wamekipiga dhidi ya mtibwa Sugar katika dimba la Uhuru jijini Dar es Salaam.
Wekundu wa msimbazi walishinda 2-0 magoli ya Simba yalifungwa na Ibrahimu Ajibu na Shiza Kichuya huku Fredrick Blagnon alikosa penalti wakati katika shamba la bibi wana jangwani wameibuka na ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Mtibwa lakini kubwa katika mechi hiyo ni mchezaji ghali chirwa kufunga goli kwa mara ya kwanza tangu atue katika klabu hiyo.
kwa matokeo hayo simba imezidi kujikita kileleni mwa msimamo kwa kufikisha pointi 20 baaada ya kushuka dimbani mara nane wakati yanga imepanda hadi nafasi ya nne na pointi 14 baada mechi saba mtibwa wako sawa na yanga wakiwa wanatofautiana magoli ya kufungwa nakufunga.
stendi united imeendeleza kuwasha moto baada ya kushinda 1-0 dhidi ya Azam stend kuendelea kushika nafasi ya pilina pointi 19 baada ya kucheza mechi tisa.
0 comments:
Post a Comment