Kocha wa The Gunners Arsene Wenger amesema anaamini kuungo fundi wa Ujerumani Mesut Ozil ataendelea kuwepo katika klabu hiyo licha ya mchezaji huyu mwenye asili ya Uturuki kutaka kulipwa pauni 200,000 kwa wiki.
![]() |
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger |
Tupo kwenye ligi yenye timu kama Manchester City Liverpool Tottenham, na Manchester United huwezi kuwa na uhakika wa kutwaa ubingwa kila mmoja anapigania nafasi hiyo,
Kwa sasa Ozil analipwa Pauni 140,000 kwa wiki na katika mchezo wa juzi dhidi ya Swansea city alifunga goli safi akimalizia krosi nzuri ilipigwa na Alexis Sanchez na siku hiyo alikuwa anashereheka kutimiza umri wa miaka 28 mkataba wa sasa utaisha 2018 kwa maana hiyo kuanzia dirisha la majira ya kiangazi atakuwa huru kuondoka.
![]() |
Mchezaji wa Arsenal (Kulia) Mesut Ozil akifunga goli kwenye mchezo wa ligi ya Epl dhidi ya Swansea City The Gunners walishinda 3-2. |
0 comments:
Post a Comment