Kocha wa Everton Ronald Koeman amemwagia sifa kibao bosi wa timu ya Manchester City Pep Guardiola lakini akamtupitia kijembe kwa kumwambia kuwa anataka kutwaa ubingwa ligi kwa njia ngumu akiimanisha soka la pasi nyingi, mfumo ambao Guardiola n muumini wa falsafa hiyo.
![]() |
Kocha wa Everton Ronald Koeman( kushoto) akitoa maelekezo kwa mshambuliaji Romelo Lukaku |
Everton watakuwa ugenini kucheza na City ambao katika dimba la Etihad mechi yao mwisho kabla ya mapumziko kwa ajili kupsha mech za kimataifa, waloja kipigo kwa mara ya kwanza baada ya kufungwa 2-0 na Tottenham Hotspurs.
Pep na Koeman ni marafiki na pia walicheza pamoja kwenye kikosi cha Barcelona miaka tisini lakini kesho wataweka urafiki wao mbembeni wakiwa wanasaka pointi tatu muhimu City anaongoza ligi akiwa na pointi 18 na Everton yupo nafasi ya 5 na pointi 14.
![]() |
Pep na Koeman walivyokuwa Barcelona |
0 comments:
Post a Comment