Search This Blog

SportsRaw

SportsRaw

Friday, 28 October 2016

Kiba: hatujashindwa,waliopata tuzo wanastahili

Staa wa Bongo fleva nchini Ali Kiba amfunguka na kuzungumzia ushiriki wa wasanii kutoka Tanzania kwenye tuzo za MTV Mama Awards 
Mkali huyo wa ngoma ya Aje  ambaye alikuwa miongoni kati ya wasanii waliotumbuiza kwenye tuzo hizo na pia aliwania tuzo ya ‘Best Collaboration’ ya wimbo wa Unconditionally Bae alioshirikiana na Sauti Sol, amesema watanzania walijitahidi lakini walizidiwa na wasanii wa nje ndiyo maana wakashindwa kutamba.

“Katika ushindani kuna kushinda na kushindwa sisi hatusemi kuwa tumeshindwa na naamini Tanzania ina vipaji sana na kila msanii anajitahidi kufanya kwa uwezo wake ili aweze kufikisha nchi yetu sehemu nzuri,” AliKiba alikiambia kipindi cha Clouds 360. “Kwasasa muziki wetu umekuwa kwa kasi sana na unazidi kuvuka mipaka yanchi yetu. Kwa washindi ambao wameshinda kwenye tuzo za ‘MTV Mama Awards’ wanastaili kwasababu kazi wamefanya na tumeziona”
Katika hatua nyingine muimbaji huyo amewataka mashabiki wa muziki wake kukaa makao wa kula kwa ajili ya ujio wa kolabo yake mpya ya kimataifa.

0 comments:

Post a Comment