Supa staa wa Real Madrid Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa ligi ya mabingwa Ulaya ambayo huandaliwa na kupigiwa kura na magezeti makubwa ya Michezo Marca la nchini Uhispania na Gazzetta Dello Sport.
Ronaldo ambae ni raia wa Ureno alifunga magoli 16 katika ligi ya Mabingwa na 51 katika michuano yote na kuisadia Madrid kutwaa kombe la hilo kwa mara ya 11 na pia kutoa mchango mkubwa katika timu ya taifa baada ya kushinda ubingwa wa kiihistoria Euro wakiishinda dhidi ya Mwenyeji Ufaransa na kuwa na nafasi kubwa ya kushinda mchezaji bora wa dunia Ballon d"Or.
Akifanya mahojiano na gazeti la Marca Ronaldo 31' amemwagia sifa kibao kocha wa miamba hiyo ya Santiago Bernabeu nimeshinda ligi ya mabigwa na Euro ni mwaka wa kihistoria kwangu kamwe siwezi kuusahau alisema Ronaldo.
Cr7 anaoopngoza katika listi ya wafumania nyavu katika ligi ya mabigwa akiwa na magoli 94 akiwa na Manchester United na Real Madrid nafasi ya pili yupo staa wa timu ya Barcelona Leonel Messi mwenye magoli 83.
Ronaldo pia amewashukuru wachezaji wenzake wa madrid na Ureno kwa kusema mafanikio alioyapata bila wao asingeyapata.
0 comments:
Post a Comment