Mchezaji wa klabu ya Barcelona, Gerard Pique ametangaza kuwa msimamo wake bado upo pale pale kuwa atastaafu kuichezea timu ya Taifa ya Hispania baada ya michuano ya kombe la Dunia 2018, Russia.
Beki huyo ameyasema hayo baada ya ushindi wa 2-0 ugenini dhidi ya Albania, mechi ambayo ilifanya mchezaji huyo kukosolewa sana kufuatia jezi aliyoivaa. Pique alivaa jezi ambayo mikononi ilikuwa haina mistari ya rangi ya bendera ya Hispania na hivyo kupingwa na kushambuliwa na mashabiki wengi hasa katika mitandao ya kijamii
Mashabiki mara nyingi wamekuwa wakimzomea mchezaji huyo kufuatia kusapoti harakati za jimbo la Catalunya ambalo limekuwa likipigania uhuru wake kutoka Hispania.

Hata Hivyo shirikisho la mpira wa miguu la Hispania “RFEF” lilitoa ufanunuzi juu ya jezi ya Pique kuwa ile mistari ya rangi ya bendera katika jezi za Adidas ipo kwa wanaotumia jezi za mikono mifupi na sio za mikono mirefu, hilo linathibitika katika jezi aliyovaa Sergio Ramos ya mikono mirefu
Shirikisho limeeleza kuwa jezi ya Gerard Pique ilikuwa ya mikono mirefu, hivyo akaikata ili ajisikie huru, kitu ambacho wachezaji wengi hukifanya.
Pique ambaye hadi sasa ameichezea Hispania mechi 85 na kufunga magoli matano, ameeleza kuwa mpango wa kustaafu baada ya kombe la dunia alikuwa nao na haujasababishwa na tukio hili.
“Nimelifikiria sana, maamuzi hayajatokana na tukio hili. Kuna watu wanafikiri ni bora tu nisiwepo hapa,” amesema beki huyo.
0 comments:
Post a Comment