Search This Blog

SportsRaw

SportsRaw

Tuesday, 18 October 2016

Kichuya mchezaji bora vpl

Mshambuliaji Shiza Kichuya wa Simba SC amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa Septemba msimu wa 2016/2017.
Image result for kichuya

Kichuya  aliwashinda wachezaji Adam Kingwande wa Stand United na Omari Mponda wa Ndanda FC.

Mchezaji aliisadia timu yake kwa mwezi huo kupata pointi zote 12 katika mechi nne ilizocheza, matokeo ambayo yameifanya Simba iendelee kuongoza Ligi hiyo inayoshirikisha timu 16. Pia alifunga mabao matatu katika mechi mbili kati ya nne ilizocheza timu yake.


Kwa kushinda tuzo hizo ya mwezi, Kichuya atazawadiwa kitita cha sh. 1,000,000 (milioni moja) kutoka kwa wadhamini wa Ligi hiyo, kampuni ya Vodacom Tanzania.

0 comments:

Post a Comment