Kocha wa Jose Mourinho  jumatatu anakutana uso kwa uso na Jurgen Klopp katika mechi ya kukatana shoka  kati  Manchester United dhidi ya majogoo wa jiji la Anfield Liverpool ambao wapo kwenye fomu kwa sasa.

hii itakuwa mara ya kwanza kwa Mourinho akiwa kama kocha wa United kukutana na Klopp lakini itakuwa mara ya sita kukutana, kuelekea mchezo huu rekodi zikoje kwa wawili hawa wanapokutana.
Borussia Dortmund  2-1  Real Madrid  October 2012
October 2, 2012 ndio siku ya kwanza iliwakutanisha makocha hao  katikamechi ya ligi ya Mabigwa ulaya magoli ya Robert Lewandowski akifungua akaunti ya magoli dakika chache baadae  Cristiano Ronaldo akazawazisha kipind cha pili   Marcel Schmalzer  akaongeza la pili nakufanya mchezo kuisha kwa 2-1.
Real Madrid 2-2 Borussia Dortmund. Novemba 2012
Mechi ya pili ya marudiano ya ligi ya mabigwa ulaya Mourinho anashindwa kupata matokeo nyumbani Santiago Bernabeu.

Borussia Dortmund  4-1 Real Madrid  Aprili 13 2013 
hii ilikuwa nusu fainali ligi ya mabigwa ulaya na mechi ya kwanza ilichezwa Signal Iduna Park Robert Lewandowski tena akapeleka maumivu kwa Mourinho na kuendeleza uteja mbele ya Klopp.
 Real Madrid  2-0 Borussia Dortmund   Aprili  2013
Kwa mara ya Kwanza Mourinho anapata ushindi nyumbani lakini matokeo hayo ya kumsaidia baada ya kukubali kichapo cha 4-1mechi ya kwanza,Madrid wanashimdwa kufuzu hatua ya fainaili ilichezwa nchini England katika dimba la Wembley

Chelsea 1-3 Liverpool Octoba 2015
hapa ilikuwa ligi kuu England kwa mara nyingine Mourinho anashindwa kupata matokeo akiwa kama kocha wa Chelsea.
kwa rekodihiyo kocha wa Liverpool amekuwa mbabe kwani ameshinda mechi 3moja ametoka sare namoja amefungwa  swali ambalo wengi wanajiuliza je je kwa mara ya sita wakikutana  Mourinho atafuta uteja au   Klopp ataendeleza utemi jibu litapatikana jumatatu.






 
 
0 comments:
Post a Comment